Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa Mwanza wamekutana na Wachimbaji wa madini Kanda ya Ziwa, wanunuzi pamoja na wauzaji wa masoko ya nje kujadili ni kwanini madini bado yanatoroshwa kupelekwa nje ya nchi?
Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Waziri Nyongo amesema toka zamani madini yamekuwa yakitoroshwa kwenda nje ya nchi kupitia njia ya Bahari na Viwanja vya ndege na utoroshaji huo umechangia kupunguza pato la Taifa.
“Madini yetu yanatoroshwa kupitia njia mbalimbali za nchi, sisi tumeona utoroshaji unachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza mapato ya nchi yetu, kama tunavyofahamu sekta ya Madini ina mchango mdogo sana tuna Madini mengi nchini lakini mchango wake ni mdogo” -Naibu Waziri Nyongo
KIGWANGALLA ATOA MIEZI 9 “KWA SASA HATUTOTUMIA NGUVU KWANZA” , BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA