Mpima ardhi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Thobias Patrick amemwaga chozi mbele ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akijitetea kuhusu tuhuma za kupima eneo la Serikali na kujimilikisha kisha kuliuza.
Hayo yametokea jana February 26, 2018 wilayani Kahama mkoani Shinyanga wakati wa ziara ya Waziri Lukuvi katika kampeni yake ya ‘Funguka kwa Waziri’ ambapo wakazi wa mji huo walimfikishia Waziri wa Ardhi tuhuma zinazomkabili afisa huyo.
Mara baada ya kupata tuhuma hizo William Lukuvi alitembelea eneo linahusishwa na tuhuma hizo na kumhoji afisa huyo kwanini alipima eneo la Serikali na kumilikisha watu binafsi na yeye akiwa mmiliki wa kiwanja kimoja wapo na kisha kukiuza.
Mpima Ardhi huyo Thobias Patrick alipata wakati mgumu kujieleza huku akitokwa na machozi na akijitetea kuwa eneo linalohusishwa na tuhuma hizo sio la kwake kwakuwa yeye aliuza kiwanja namba 590 Block N na sio hicho anachotuhumiwa kukiuza.
Wanafunzi waandamana Mwanza wakitaka warudishiwe Elfu 50 zao
“Wewe tuliyekupa leseni ya kuuza madini nje, unaenda kuuzia wapi?” Naibu Waziri wa Madini