Leo February 27, 2018 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe amezungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza toka uchaguzi wa marudio kwenye majimbo ya Kinondoni na Siha ufanyike mwezi huu.
Katika mkutano huo Mbowe amesema kuwa leo ataambatana na Viongozi wengine 6 wa CHADEMA wataenda kuripoti Kituo cha Polisi cha Kati ili kutii wito.
Ameeleza kuwa tangu tamko la polisi limetolewa Katibu wa Mkuu wa CHADEMA Dr. Vincent Mashinji ambaye pia alitakiwa kuwa mmoja wao kwenye kuripoti polisi, yuko nje ya nchi hivyo hatokuwa nao lakini akirejea atakwenda kuripoti.
“Hatutakataa wito wa polisi wakati wowote kwasababu sisi sio wahalifu na kwasababu sio wahalifu hatuna sababu ya kukimbia, japo tunajua wanachopanga juu yetu, hatutaogopa polisi, wala uongozi wowote, tutaiheshimu nchi na sheria zake na kutetea haki za taifa hili.” -Mbowe
Mpima ardhi amwaga chozi mbele ya Waziri Lukuvi
Wanafunzi waandamana Mwanza wakitaka warudishiwe Elfu 50 zao