Shirika moja la habari nchini Austria lijulikanalo kama ORF limefungua mashtaka dhidi ya Makamu wa Rais wa nchi hiyo baada ya kiongozi huyo kulituhumu shirika hilo la habari na mtangazaji wake mmoja kuwa ni waongo.
Makamu huyo wa Rais Heinz-Christian Strache alitoa tuhuma hizo juzi kwenye mtandao wa Facebook huku akisema kuwa chombo hicho kinafanya kazi kwa upendeleo na anataka kufuta sera ya kutokitoza kodi chombo hicho cha habari.
Mtangazaji Armin Wolf ambaye pia ameungana na shirika hilo kufungua mashtaka dhidi ya kiongozi huyo amesema kuwa hajawahi kuambiwa na mwanasiasa yeyoye kuwa yeye ni muongo.
Wanafunzi waandamana Mwanza wakitaka warudishiwe Elfu 50 zao
Mbowe na Viongozi wengine wa CHADEMA walivyofika Polisi kuripoti