Teknolojia inazidi kukua ulimwenguni kote kila siku ikiwa ni matokeo ya kuvumbuliwa kwa vitu, mifumo, vifaa na vitu vingine vipya ambavyo ni vya teknolojia za juu zaidi kuliko vilivyopo.
Kutoka nchini Ujerumani, miji ya nchi hiyo itaanza kupiga marufuku magari ya zamani yanayotumia dizeli, hii ni kufuatia maagizo mapya ya Mahakama.
Mahakama ya Utawala ya Shirikisho huko Leipzig imesema kuwa miji ya Stuttgart na Duesseldorf ya nchini humo inaweza kupiga marufuku magari ya zamani zaidi na ambayo yanaharibu mazingira katika maeneo yaliyoathirika na uchafuzi wa mazingira.
Uamuzi huo uliofanywa na mahakama hiyo umekuja baada ya majimbo ya Ujerumani kukata rufaa inayopinga utekelezwaji huo ambao tayari ilikuwa unafanywa na mahakama hizo za mwanzo za Stuttgart na Duesseldorf.
Fatma Karume na Mtoto wa Chacha Wangwe kufungua Kesi kupinga Wakurugenzi kusimamia Uchaguzi
Mbowe na Viongozi wengine wa CHADEMA walivyofika Polisi kuripoti