Leo February 27, 2018 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde, ameagiza waajiri ambao hawajajisajili na mfuko wa fidia kwa Wafanyakazi kufanya hivyo, vinginevyo wafikishwe mahakamani kwa kutokufanya hivyo.
Ripoti zinaonyesha kuwa jiji la Mwanza lina waajiri 1228, lakini kati ya hao ni waajiri ni 482 tu ndio waliojisajili na mfuko huku waajiri wengine 746 wakiwa bado hawajajisajili, baada ya kufanya ziara Naibu Waziri Anthony Mavunde na Mkuu wa Oparesheni wakazungumza na Wanahabari.
“Naomba ieleweke kwaajili ya wote kinachofanyika sio njia ya kuwadhalilisha watu, haya ni masharti na matakwa ya sheria yameelekeza waajiri wote lazima wajisajili, ukijisajili mfanayakazi akipata matatizo WCF ndo wanabeba jukumu,” -Naibu Waziri Mavunde
AGIZO LA WAZIRI JAFO KWA MAAFISA ELIMU WOTE NCHINI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA