Baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Neymar kuumia akiitumikia timu yake ya Paris Saint Germain ya Ufaransa, doctor wa timu ya taifa ya Brazil amelazimika kwenda Paris kumfanyia uchunguzi wa kina Neymar licha ya kuwa PSG ndio watatoa kauli ya mwisho kuhusu hali ya staa huyo.
Hata hivyo kocha wa PSG Unai Emery anazidisha matumaini kwa mashabiki wa Neymar kwa kuwaambia wapuuzie taarifa kuwa Neymar atahitaji upasuaji kama inavyoripotiwa lakini anahitaji mapumziko na week ijayo anaamini atakuwepo uwanjani kuichezea PSG dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa Champions League.
Pamoja na kuwa doctor wa timu ya taifa ya Brazil amesafiri kwenda Paris kufuatilia hali ya Neymar anayesumbuliwa na jeraha la mguu wake wa kulia eneo la karibu na enka, anazidisha hofu wasije kumkosa katika World Cup 2018 lakini mkurugenzi wa ufundi wa chama cha soka cha Brazil Edu Gaspar wataheshimu mtazamo au ripoti ya jopo la madaktari wa PSG pamoja na wao kumtuma doctor wao.
Taarifa za majeraha ya Neymar ambayo yanaipa presha Brazil yanakuja ikiwa imesalia miezi minne tu kabla ya Brazil kutupa karata yake ya game ya ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia 2018 inayofanyika nchini Urusi, Brazil ikitarajia kucheza mchezo wa ufunguzi June 17 2018 dhidi ya Switzerland. Neymar aliumia mguu wake wa kulia karibu na enka siku ya Jumapili dakika ya 77 wakati wa game dhidi ya Marseille iliyomalizika kwa PSG kupata ushindi wa magoli 3-0.
VIDEO: Kocha msaidizi Simba baada ya kudaiwa kutopewa mkono na Ndemla