Leo February 28, 2017 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wazazi na walezi wa watoto wenye mahitaji maalumu kutowafungia ndani na badala yake wawapeleke shule.
Waziri Mkuu Amesema ulemavu si kigezo cha kuwakosesha watoto hao kupata elimu na kufanya kazi, hivyo amewataka jamii kutowakatisha tamaa
Ametoa agizo hilo wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa majengo ya chuo cha Ualimu Kitangali, kilichopo Newala mkoani Mtwara.
“Watakaobainika kuwafungia ndani watoto wenye mahitaji maalumu wachukuliwe hatua za kisheria kwa sababu wanawakosesha haki ya kupata elimu.” -Waziri Mkuu Majaliwa
Waziri Mkuu alisema Serikali inataka watoto wenye mahitaji maalumu watambulike pamoja na mahitaji yao na waliofikia umri wa kwenda shule wapelekwe.
“Tunataka kila mtoto wa Kitanzania aliyefikia umri wa kwenda shule apelekwe shule na kusoma na wenzake. Serikali imeboresha elimu ili watoto wote wasome” -Waziri Mkuu Majaliwa
AGIZO LA WAZIRI JAFO KWA MAAFISA ELIMU WOTE NCHINI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA