Leo February 28, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru wafuasi 7 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao ya kuwapiga mawe Polisi na kulizuia Jeshi hilo kutekeleza majukumu yake.
Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amesema mashahidi watatu wa upande wa mashtaka wametoa ushahidi hafifu ambao hauwezi kuwatia hatiani washtakiwa.
“Hivyo ushahidi umeshindwa kuwatia hatiani washtakiwa nawaachia huru,” amesema Hakimu Simba.
Walikuwa wanakabiliwa na kesi ya kufanya fujo ambapo inadaiwa January 6, 2015 waliwapiga mawe Polisi na kuwazuia kutekeleza majukumu yao maeneo ya Ubungo Riverside.
FULL VIDEO: SUGU NA MASONGA WAKIPELEKWA GEREZANI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA