Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza rasmi leo February 28, 2018 marufuku kwa vyombo vya habari nchini kupiga nyimbo 13 za bongofleva ambapo mamlaka hiyo imedai kuwa nyimbo hizo hazina maadili.
Taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo inaeleza kuwa ilipokea orodha ya nyimbo hizo kutoka kwa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) ambalo limeeleza kua nyimbo hizo ni kinyume na maadili na kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) 2005.
Baadhi ya nyimbo hizo zilizofungiwa ni pamoja na Wakawaka na Hallelujah za Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, Kibamia wa Roma Mkatoliki, Hainaga ushemeji wa Amani Hamis maarufu kama Manfongo, Nimevurugwa wa Snura Mushi maarufu kama Snura na nyingine.
Madiwani wawili wa CHADEMA wajiuzulu Serengeti kuhamia CCM