Leo February 28, 2018 Mahakama ya kijeshi nchini DRC Congo imemfunga kifungo cha maisha jela ofisa wa polisi aliyemuua kwa kumpiga risasi mshiriki wa maandamano ya kumpinga Rais Joseph Kabila.
Pia Polisi ambaye alimpiga risasi mwanaharakati Rossy Mukendi wa kundi la Collective 2016 katika jiji la Kinshasa amekamatwa, amesema msemaji wa polisi Kanali Pierrot-Rombaut Mwanamputu.
Mukendi alifariki kutokana na majeraha, hali iliyosababisha kundi jingine liitwalo Chama cha Kutetea Upatikanaji Haki za Wacongo kusema “mauaji” hayo yalipangwa.
Lakini ofisa usajili katika mahakama ya kijeshi kaskazini magharibi mwa DRC aliliambia shirika la AFP: “Ofisa wa polisi Agbe Obeid amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kumpiga risasi kwa karibu na kumuua Eric Boloko Jumapili, February 25, eneo la Mbandaka.”
Naye Fabien Mongunza, rais wa chama cha kiraia katika jimbo la Ikweta amesema “Huyu polisi anayefurahia mtutu alimuua mtu ambaye alikuwa anakwenda nyumbani (baada ya maandamano). Natumaini kwamba atatumikia kifungo chote.”
“Hukumu hiyo imetuliza nyoyo za watu kwa sababu chuki ilikuwa ikionekana wazi. Jaji wa kijeshi amefanya vema kumtia hatiani haraka polisi huyo.” -Mongunza
WALIOJERUHIWA KWA RISASI MAANDAMANO YA CHADEMA WAFIKISHWA MAHAKAMANI