Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango leo February 28, 2018 ameeleza kuwa mwaka huu 2018 inakadiriwa kuwa idadi ya watu nchini itaongezeka hadi kufikia watu Milioni 54.2 ambapo kati yao Milioni 52.6 ni Tanzania bara.
Dr. Mpango ameeleza kuwa idadi hii inakadiriwa kufikia Milioni 59.4 ifikapo mwaka 2021 na hivyo Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano unamalizika mwaka 2021, serikali inapoandaa mpango huo wa awamu ya tatu utandaa kwa kujua nchi ina watu takribani Milioni 60.
Waziri Mpango ameeleza kuwa ifikapo mwaka 2030 nchi inakadiriwa kuwa na watu milioni 77.5 na huu ndio mwaka ambao itafanyika tathmini ya utekelezaji wa malengo ya Mpango wa Dunia wa Maendeleo Endelevu (SDGs).
“Kwa kuzingatia matokeo ya sensa ya maendeleo ya watu na makazi ya mwaka 2012, inakadirika kuwa kila mwaka kuna ongezeko la wastani wa watu milioni 1.6 nchini.” – Waziri Mpango
Madiwani wawili wa CHADEMA wajiuzulu Serengeti kuhamia CCM
Waliopigwa risasi maandamano ya CHADEMA waachiwa kwa dhamana