Rais wa zamani wa club ya FC Barcelona ya Hispania Joan Laporta anaamini kuwa Arsenal wanaweza kuiga mfano wa FC Barcelona kumteua staa wao wa zamani Thierry Henry kuwa kocha wao kama ambavyo Barcelona waliwahi kufanya hivyo kwa Pep Guardiola na walifanikiwa kupata mataji mbalimbali.
Pep Guardiola akiwa na umri wa miaka kwa sasa anatajwa kama moja kati ya makocha bora duniani, kitu ambacho kilichangiwa na club ya FC Barcelona kumuamini na kumpa nafasi na inaaminika kuwa Thierry Henry anaweza kupita huko na kufanikiwa kama tu uongozi wa club ya Arsenal utakubali kumuamini na kumpa timu.
Joan Laporta amefikia hatua ya kusema hivyo akidai kuna vitu vingi ambavyo anaviona vinashabihiana kati ya Pep Guardiola na Thierry Henry, hivyo anaona itapendeza kama Arsenal watamtazama Henry kama kocha wao ajaye baada ya Arsene Wenger, kama hufahamu Joan Laporta amewahi kuwa Rais wa FC Barcelona kwa miaka 7 kuanzia (2003-2010).
“Nafahamu kuwa Thierry Henry anaipenda Arsenal na anawapenda na mtu mwenye tabia nzuri na makini katika kile kitu anachokifanya na muwajibikaji, kama atahitaji kuwa kocha lazima atapenda kuifundisha Arsenal kwa sababu anashawishika nayo hivyo atafanya nayo vizuri”>>>Joan Laporta
VIDEO: Kocha msaidizi Simba baada ya kudaiwa kutopewa mkono na Ndemla