Baada ya jopo la madaktari wa club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa na jopo la madaktari wa timu ya taifa ya Brazil kwa kushirikiana kukaa na kumfanyia uchunguzi wa kina Neymar, leo wamefikia makubaliano ya kumfanyia upasuaji staa huyo baada ya kuona hakuna njia mbadala ya kutatua tatizo lake zaidi ya upasuaji.
Neymar aliumia mguu wake wa kulia karibu na enka siku ya Jumapili dakika ya 77 wakati wa game dhidi ya Marseille iliyomalizika kwa PSG kupata ushindi wa magoli 3-0 lakini baada ya jopo la madaktari kufanya uchunguzi imebainika staa huyo anahitaji upasuaji ili kupona, ila upasuaji wake utamuweka nje ya uwanja kwa miezi miwili, upasuaji wa Neymar utafanyika wiki hii nchini kwao Brazil.
Ikumbukwe tu zimesalia siku 109 kabla ya Brazil kucheza game yake ya ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia 2018 inayofanyika nchini Urusi, Brazil ikitarajia kucheza mchezo wa ufunguzi June 17 2018 dhidi ya Switzerland lakini taarifa hizo ni pigo kwa klabu ya PSG anayichezea Neymar kwani sasa ni rasmi watamkosa katika mchezo wa marudiano wa Champions League dhidi ya Real Madrid wiki ijayo.
VIDEO: Ni Ray vs JB ulingoni April 1 2018, JB ametangaza kulinda rekodi yake