Jeshi la Polisi huko Trans Mara katika mji wa Kilgoris nchini Kenya wameanza uchunguzi na kumtafuta kijana mmoja ambaye anadaiwa kumchoma kisu hadi kufa mwanafunzi wa kidato cha kwanza jana February 28, 2018.
Inaelezwa kuwa mtuhumiwa huyo anayejulikana kama Hillary Langat alikuwa mfanyakazi wa mama mzazi wa mtoto huyo na alikwenda nyumbani kwa bosi wake huyo mida ya saa 3 asubuhi na kumkuta mtoto huyo ambaye alikuwa likizo.
Langat alimchoma kisu tumboni mtoto huyo na kisha kukimbia. Kwa mujibu wa polisi
Langat ambaye alikuwa ni dereva wa mama wa mtoto huyo, alifukuzwa kazi wiki chache zilizopita na hivyo alirudi kufanya tukio hilo kwa mtoto wa boss wake kama kulipa kisasi kwa kufukuzwa kazi.
Nyimbo 13 za Bongofleva, TCRA imeagiza zisipigwe Redioni wala TV
Lundenga ajiondoa MISS TANZANIA