Kama umewahi kutazama Live Show maarufu ya Big Brother, utakuwa unafahamu hata kwa uchache maisha wanayoishi washiriki wa show hiyo kutoka nchini mbalimbali za Afrika. Ni namna ya jinsi kila mmoja wao anavyoishi ndiyo huwapelekea aidha kutolewa kwa kura za watu au kuendelea na mashindano hayo.
Katika hali iliyoibua hisia za watu mbalimbali wanaofuatilia show hiyo kwa nchi ya Nigeria yaani Big Brother Naija, siku tatu tu baada ya kamera kuwanasa washiriki Bambam na Teddy A wakifanya mapenzi chooni, wazazi wa Bambam wameonesha kuchukizwa na kitendo hicho.
Habari kutoka Nigeria ni kwamba wazazi hao wameeleza kusikitishwa kwao na suala hilo na wameomba mtoto wao huyo Bambam kurudishwa nyumbani na kuachana na mashindano hayo.
Kwa mujibu wa binti aliyedai kuwa ni rafiki wa Bambam na familia zao zimekuwa marafiki kwa muda mrefu aitwaye Fisayo Awunoga, wazazi wa Bambam wamekasirika sana na wameshakutana na uongozi wa shindano hilo na kuomba afukuzwe vinginevyo binti huyo asionekane akifanya mapenzi tena akiwa kwenye shindano hilo.
Lundenga ajiondoa MISS TANZANIA
‘Quick Rocka hanipangii cha kufanya, ananisikiliza ninachomwambia’