Leo March 1, 2018 Kumetokea hali ya taharuki katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar Es Salaam baada ya kutokea kwa mlipuko wa moto uliosababishwa na Transfomer.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mtendaji wa Mahakama hiyo, Gasto Kanyairita amesema kuwa moto huo umetokea majira ya saa 4 asubuhi.
Amesema kuwa wakati mlipuko huo unatokea kulikuwa na kesi nyingi zikiendelea mahakamani.
“Baada ya kufatilia tulibaini kuwa ni transformer ambapo ilisababisha kuungua kwa waya wa TTCL, simu na Internet ambapo shughuli za mahakama zilisitishwa kwa muda,” -Gasto Kanyairita
Pia amesema shughuli za mahakama zinaendelea ambapo Data za kesi zipo salama.
“Niwatoe hofu Watanzania mlipuko uliotokea ni wa shoti ya umeme na ni kawaida kutokea, hivyo waepukane na taarifa za uongo,”-Gasto Kanyairita
Mmoja wa mashuhuda tukio hilo, amebainisha kuwa walisikia kishindo kikubwa cha mlipuko ambapo iliwabidi wakimbizane kutoka nje ya mahakama.
“Ilitubidi tutoke nje kutokana na hofu tuliyokuwa nayo, lakini tunashukuru hakuna madhara yoyote ya kibinadamu,”-Shuhuda
WAFUASI 7 WA CHADEMA WASHINDA KESI DAR ES SALAAM, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA