March 1, 2018 Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo alikutana na wadau mbalimbali wa sekta ya afya ofisini kwake Dodoma lengo likiwa ni kubaini changamoto zinazoikabili sekta hiyo pamoja na kushauriana namna ya kuzitatua.
Katika hitimisho lake Waziri Jafo hakuacha kuzungumzia tatizo la baadhi ya wazazi kuacha kuwanyonyesha watoto wao kwa kuogopa kuwabemenda pindi wanapopata mimba nyingine ambapo amesema…>>>“Mtu anakuambia mama akipata ujauzito wakati ananyonyesha anambemenda mototo na kwasababu wazazi hawana elimu basi akipata ujauzito mama anamkatisha mototo kunyonya” –Waziri Jafo
“Ndio maana leo watoto wanapelekwa kwa bibi, mama anaona aibu kumlea mototo kwa madai amembemenda. Ile ni hali ya homoni ambayo inabadilika kwa muda na mototo anarejea katika hali ya kawaida”-Waziri Jafo
TCRA imezindua mfumo wa usajili laini kwa kutumia alama za vidole