Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Rose Muhando alikuwa kimya kwa zaidi ya miaka mitano sasa bila ya kutoa album yoyote tofauti na miaka ya nyuma, kitu ambacho kilipelekea mashabiki wake kumiss album ya nyimbo zake baada ya kimya hicho.
Rose Muhando baada ya kimya hicho February 22 2018 ilitangazwa siku atakayoachia album yake mpya ya nyimbo za injili kuwa ni April 1 2018 siku ya sikukuu ya Pasaka katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Kuelekea uzinduzi huo ambao utakaofanywa kwenye tamasha la Pasaka, waandaaji wametaja kuwa list ya wasanii wa Injili watakaopanda katika stage ni wengi lakini muimbaji wa kimataifa kutokea Zambia Ephraim Sekeleti amethibitisha kuwa atakuwa jukwaa moja na Rose Muhando.
VIDEO: Naibu waziri alivyoeleza sababu za kumfungia Roma na kumpa onyo Nay wa Mitego