Taasisi ya ISDI leo Alhamisi ya March 1 2018 imeanza kutoa mafunzo maalum kwa viongozi wa vilabu vya Ligi Kuu na Ligi daraja la kwanza kwa ajili ya kuleta mapinduzi ya utawala katika soka hususani kuviwezesha vilabu kujitegemea katika mfumo mzima wa utawala na utendaji.
Mafunzo hayo yamekuja baada ya tafiti zilizofanywa kwa muda mrefu na ISDI na kubaini changamoto zilizopo katika vilabu vya soka vya Ligi Kuu na Ligi daraja la kwanza, hivyo wameanza kwa kutoa mbinu za kuvikomboa vilabu hivyo.
Taasisi ya ISDI inayoongozwa na mwenyekiti wake DR TM Katunzi, katibu mkuu wa zamani wa Yanga Dr Jonas Benedict Tiboroha ambaye ni mkurugenzi kwa kushirikiana na katibu wa taasisi hiyo Peter Simon huku Rais wa TFF Wallace Karia akitia baraka mafunzo hayo.
Ajenda kubwa iliyojadiliwa katika semina hiyo ni kujenga uelewa kwa viongozi wa vilabu vya Ligi Kuu na Ligi daraja la kwanza namna ya kutatua changamoto za vilabu vyao ambavyo kwa asilimia kuwa vingi wao ni tegemezi na utawala wao umegubikwa na migogoro na changamoto mbalimbali.
https://youtu.be/uat3cR3W2QQ
VIDEO: Naibu waziri alivyoeleza sababu za kumfungia Roma na kumpa onyo Nay wa Mitego