Kamanda wa Polisi Dodoma Gilles Muroto leo March 2, 2018 alikutana na waandishi wa habari na kuwaeleza kuhusu misako iliyofanywa na jeshi lake ambapo imewakamata baadhi ya waalifu wakiwemo wahamiaji haramu, wasafirishaji mali za magendo pamoja na watengenezaji bima feki.
Kamanda Muroto amesema …>>>”Tukio la kwanza tumewakamata watu sita kwa kosa la kusafirisha mali kwa lengo la kuiba. Mali hiyo ni roller nane za malighafi za mabati zilizokuwa zikisafirishwa kutoka katika kiwanda cha mabati cha ALAF kwenda Kigali”
“Tukio lingine tumewakamata wahamiaji haramu wawili katika check point ya Polisi Mtera Wilaya ya Mpwapwa Dodoma katika barabara kuu ya Dodoma-Iringa. Wahamiaji hao walikuwa wakisafirishwa katika roli la mizigo aina ya Mitsubishi. Katika Operesheni nyingine tumekamata magari yanayotumia bima za bandia na yasiyo na bima ambapo jumla ya magari 15, Pikipiki 2 na bajaji 5”-Kamanda Muroto
“Watu hawana elimu kuhusu KUBEMENDA watoto” –Waziri Jafo