Bibi harusi mmoja ameamriwa na Mahakama nchini Uingereza alipe fidia ya Dola 115,000 sawa na Tshs Milioni 276 kwa kuichafua kampuni ya kupiga picha ya Amara Wedding kwenye mtandao.
Inaelezwa kuwa Bibi Harusi huyo anayejulikana kwa jina la Emily Liao hakuridhishwa na picha zilizopigwa na kampuni hiyo kabla ya siku ya harusi yenyewe, yaani Pre-Wedding photos na hivyo akaanzisha kampeni ya mtandaoni ya kuchafua jina la kampuni hiyo.
Emily alitumia kama mwaka mzima kusemea vibaya huduma zinazotolewa na kampuni hiyo ya picha jambo lililosababisha kampuni hiyo kufunga biashara January 2017 .
Katika mitandao yake ya kijamii Emily ambaye ana asili ya Canada aliwatuhumu AmaraWedding na mmiliki wake Kitty Chan, kwamba walikuwa wakitumia njia ovu na kudanganya wateja wao
BREAKING: Baadhi ya Viongozi wa ACT Wazalendo wahamia CCM
Naibu waziri alivyomfungia Roma leo na kumpa onyo Nay wa Mitego