Jumuiya ya Taasisi ya Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) leo Jumamosi ya March 3, 2018 imetoa tamko tangu kutokea kwa kifo cha mwanafunzi wa Chuo Cha Usafirishaji (NIT) Akwilina Akwilini February 16, 2018 aliyeuawa na risasi.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari njini Dodoma Mwenyekiti wa TAHLISO George Albert Mnali ameeleza kwa niaba ya Baraza Kuu la Jumuiya hiyo ambalo linahusisha Marais wote wa serikali za wanafunzi kwenye vyuo vikuu vyote nchini wamesikitishwa na suala la vikundi vya wanafunzi kutoa matamko mbalimbali kuhusu kifo cha mwanafunzi Akwilina.
Ameeleza kuwa vikundi vingine vilienda mbali zaidi na kuwataka baadhi ya watendaji wa serikali wajiuzulu ikiwa ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr Mwigulu Nchemba, jambo ambalo jumuiya hiyo imelitafsiri kama vikundi hivyo kutumika na makundi ya kisiasa.
Mnali ameeleza kuwa haiwezekani kutaka watendaji wa serikali wajiuzulu wakati uchunguzi bado unafanyika na matokeo ya uchunguzi huo bado hayajatoka.
“Jamii itambue kuwa TAHLISO ndicho chombo cha kuwasemea wanafunzi wote wa vyuo vya elimu ya juu Tanzania na sio kikundi, kingine chochote.” – George Albert Mnali
Mwishoni ametoa wito kwa wanafunzi kuendelea kuwa watulivu huku wakisubiri matokeo ya uchunguzi unaofanyika juu ya tukio hilo na kujiepusha na maandamano au vitendo vyovyote vitakavyopelekea uvunjifu wa amani.
Mwanafunzi wa CBE adaiwa kurushwa gorofani
Picha iliyomsumbua Nape Nnauye muda wote