Maduka ya supermarket nchini Afrika Kusini hivi karibuni wameanza kuondoa kwenye maduka hayo soseji ambazo zimepigwa marufuku nchini humo kutokana na kudaiwa kuwa soseji hizo zina sumu baada ya kusababisha vifo vya watu 180.
Serikali imeeleza kuwa soseji hizo zina sumu aina ya listeria hivyo kutoa onyo kwa raia wake kuepuka kula nyama za aina zote ambazo zimeshatengenezwa na ziko tayari kuliwa tu. Wateja waliokuwa wamenunua soseji hizo wamezirudisha huku wengine wakihitaji pesa zao zirudishwe.
Inaelezwa kuwa madhara yaliyosababishwa na soseji hizo yamegundulika baada ya kuathiri watu wengi katika kipindi cha mwaka mmoja.
Magari 10 yanayoongoza kwa kununuliwa na Watanzania
HEKAHEKA: Chatu asababisha Wanaume kulala nje ya ndoa zao DSM