Muimbaji wa gospel Rose Muhando wote tunafahamu kuwa alikuwa kimya kwa zaidi ya miaka mitano sasa bila ya kutoa album yoyote tofauti na miaka ya nyuma, kitu ambacho kilipelekea mashabiki wake kumiss album ya nyimbo zake sokoni baada ya kimya hicho.
Rose Muhando baada ya kimya hicho sasa ni rasmi atazindua album yake mpya ya nyimbo za injili baada ya kimya cha muda mrefu, siku ya April 1 2018 sikukuu ya Pasaka katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Baada ya Solomon Mkubwa raia wa Congo anayeishi Kenya kuthibitisha kuwa atakuwepo katika uzinduzi huo, Ephraim Sekeleti wa Zambia na Danny M wa Kenya kuthibitisha kupanda katika stage moja na Rose Muhando, waimbaji wengine wamethibitisha leo kujumuika pamoja na Rose Muhando.
Ephraim Sekeleti kutoka Zambia ametajwa kwenye uzinduzi wa Rose Muhando