Mbunge wa Jimbo la Monduli Julius Kalanga amezungumza na waandishi wa habari leo March 5, 2018 na kusema kuwa maji yamekuwa ya shida katika wilaya ya Monduli baada ya Shirika la Umeme (TANESCO) kukata umeme kwenye chanzo cha maji Ngaramtoni kwa kudaiwa deni na TAMISEMI ambalo ni zaidi ya Tshs Milion 115.
Akizungumzia suala hilo Mbunge huyo amesema wananchi hawahusiki na malipo hayo na kinachotakiwa kifanyike ni deni hilo kulipwa ili huduma hiyo irudishwe haraka iwezekanavyo na kuepusha kadhia zaidi kwa wananchi ya maji.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TANESCO mkoa wa Arusha Donasiasa Shamba amesema wamekata umeme katika eneo hilo kwa deni la zaidi ya Tshs Milioni 115 ikiwa ni pamoja na deni la nyuma na kusema baada yakuomba wameanza kupata maji leo ambapo wamepewa wiki moja kuhakikisha wanakamilisha deni hilo la sivyo watakatiwa tena maji.
HEKAHEKA: Chatu asababisha Wanaume kulala nje ya ndoa zao DSM
Taarifa Rasmi ya CHADEMA kuhusu kulazwa kwa Mbowe