Bila shaka umewahi kusikia sheria mbalimbali za kukataza baadhi ya huduma au bidhaa kupewa au kuuzwa kwa watoto wa chini ya miaka 18, kama kuruhusiwa kuingia klabu, au kutumia vilevi na mengineyo.
Kutoka nchini Uingereza, serikali ya nchi hiyo imepiga marufuku kuuzwa kwa bidhaa za vinywaji vya sukari na kafeini (caffaine) kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 16.
Inaelezwa kuwa kutokana na marufuki hiyo maduka yatapunguza mauzo ya vinywaji vyenye zaidi ya gramu 150 ya kafeini kwa kila lita kwa kundi hilo lililotajwa.
Maduka ya supermarkets yameshaanza kutekeleza agizo hilo ambalo linaelezwa kulenga kuwafanya watoto kuishi maisha ya afya zaidi kwa kuepuka kunywa vinywaji hivyo. Hii pia itaondoka suala la watoto kupendelea kunywa vinywaji ya kuongeza nguvu ‘energy drinks’.
BREAKING: Taarifa kuhusu kutoonekana kwa Mwanafunzi Abdul Nondo
Shamba la Miti ya mbao lapandwa ya kivuli mradi wa TASAF