Tume ya kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS) jana March 6, 2018 imetoa ripoti mpya ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI nchini ambapo ripoti hiyo imeeleza kuwa jumla ya watu 225 huambukizwa VVU kila siku.
Akitoa ripoti hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dk. Leonard Maboko ameeleza kuwa hali hiyo inaonesha kuwa watu 6,750 huambukizwa kila mwezi huku 81,000 huambukizwa kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Dk. Maboko alieleza kuwa hali hii ya maambukizi ni mbaya zaidi kwa vijana katika ya miaka 15 na 24 ambapo asilimia 40 ya maambukizi mapya hutokea kwa vijana wa kundi hili la umri, na wengi wao wakiwa wanawake.
LHRC wafafanua hoja za NEC dhidi ya tamko la asasi za Kiraia
Mbunge alivyoongoza Wananchi kuua Tumbili Jimboni