Asubuhi ya leo March 7, 2018 kumesambaa video ambayo ilikuwa ni kipande cha mahojiano baina ya mtangazaji wa kituo kimoja na television na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo katika kipindi TV hiyo na video hiyo kuleta gumzo mtandaoni.
Waziri Jafo kwenye mahojiano hayo alitaja kifaa kinachopatikana maabara kinachoitwa U-tube na kusambaa kwa video hiyo kulitokana na watu kuhisi Waziri Jafo amekosea na amemaanisha mtandao wa YouTube na ndipo suala hilo lilipozua mijadala.
Kutokana na hilo Ayo TV na millardayo.com imemtafuta Waziri Jafo ambaye ameeleza kuwa hakukosea kusema neno hilo la U-tube, bali alimaanisha kifaa kinachotumika maabara kipindi akifafanua jinsi shule kongwe nchini zilivyo kwenye hali mbaya ya mpaka serikali ya awamu ya 5 imeamua kuzifanyia ukarabati.
“Hapo awali shule hizo unaweza ukakuta vifaa vya maabara ni chakavu, mfano Bunsen Burner na U-tube iliyokuwa inatumika miaka ya 80 zimechakaa mpaka kupoteza ubora wake lakini bado zinatumika mpaka sasa. Ndio maana serikali imeamua kuboresha shule hizo kongwe ili ziweze kurudi katika ubora wake.” – Waziri Jafo
Waajiri 6907 DSM kupelekwa Mahakamani
LHRC wafafanua hoja za NEC dhidi ya tamko la asasi za Kiraia