Leo March 7, 2018 Watu saba akiwemo raia wa Zambia wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji fedha wa dola za kimarekani 54,180 sawa na Milioni 120.5.
Wakili wa serikali Mwandamizi Mutalemwa Kishenyi na Mwanaamina Kombakono wamemueleza Hakimu Mkazi Mkuu Huruma shaidi kuwa washtakiwa wana makosa matatu.
Wakili Kombakono amewataja washtakiwa hao kuwa ni Robert Christopher (26)wakala wa usafirishaji mizigo, Isihaka Ngubi (25) Dereva na Cathbeth Mluga (35) ni Mlinzi wa Zambia Cargo.
Wengine ni Mrisho Mindu Karani wa kampuni ya Ulinzi Mofal, Giften John(32), Maulid Said(40) karani na Kirb Ngadu ambae ni Meneja Mwendeshaji wa kampuni ya Zambia Cargo and logistic Ltd.
Akiwasomea mashtaka yao, Kombakono amedai kuwa kosa la kwanza ni kula njama ambapo walilitenda kati ya January 26,2018 na February 6,2018 wakiwa Zambia Cargo and logistic Ltd jijini Dar es Salaam walikula njama na kutenda kosa la wizi.
Pia wanadaiwa kati ya January 26,2018 na February 6,2018 jijini Dar es Salaam waliiba katoni 700 za korosho zilizobanguliwa zenye thamani ya dola za kimarekani 54,180 sawa na Milion 120.5 mali ya Barabara Trading Tanzania Limited.
Pia kosa la utakatishaji fedha wanadaiwa wametenda kati ya January 26,2018 na February 6,2018 jijini Dar es Salaam, ambapo walijihusisha na muamala unaohusiana na katoni 700 za korosho zenye thamani ya Sh.Milion 120.5 Huku wakijua mali hiyo ni zao lilitokana na kosa la wizi.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo watuhumiwa walikana mashtaka hayo, ambapo walirudishwa rumande kwasababu shtaka la utakatishaji fedha halina dhamana kwa mujibu wa sheria.
Wakili Kishenyi amedai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi March 9,2018.
WAO WAMETUMA SALAMU KALI SANA KWA KUUA “WATU WETU WANAOVUA SAMAKI”
WAAJIRI 6907 DSM KUPELEKWA MAHAKAMANI