Tatizo la ndoa za utotoni linaendelea kutajwa kuwa desturi iliyokithiri katika jamii nyingi duniani hususani katika bara la Afrika na Asia ambapo watoto hunyang’anywa haki zao za elimu, afya, na kukosa fursa ya kukua vizuri kwa ajili ya kuozwa.
Japokuwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) siku ya jana March 7, 2018 kutoa ripoti inayoeleza takribani ndoa za utotoni Milioni 25 zimezuiwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita duniani kote, elimu bado inatakiwa kuendelea kukomboa jamii hizo.
Huko India mtoto mmoja ajulikanaye kwa jina la Monica mwenye umri wa miaka 13, amechukuliwa kama mfano baada ya kutoa taarifa kwa vyombo husika kuwa alikuwa anataka kuozwa.
Siku hiyo ya harusi ambayo kila mtu alikuwa amejiandaa na maandalizi yakiendelea, huku mtoto huyo akiwa ameanza kupambwa na kuvalishwa kwaajili ya harusi hiyo, huku saa chache zikiwa zimebakia ili aolewe alitoka nje na kupiga namba 1098.
Namba hii ilikuwa ni ya kuomba msaada wa dharura ya kwamba alikuwa anataka kuozwa akiwa na miaka 13 japo kuwa wazazi wake huwa wanawaambia watu kuwa ana miaka zaidi ya 17.
Shamba la Miti ya mbao lapandwa ya kivuli mradi wa TASAF
BREAKING: Taarifa kuhusu kutoonekana kwa Mwanafunzi Abdul Nondo