Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile siku za hivi karibuni ameeleza kuwa utafiti uliofanya katika Hospitali ya Bugando Mwanza umeonesha kuwa asilimia 83 ya wagonjwa wa Kisukari, wana matatizo sugu ya Figo pia.
Ameeleza kuwa kati ya hao wote wenye matatizo sugu ya figo asilimia 25 wanahitaji huduma za usafishaji damu na hii ni kutokana na figo kushindwa kufanya kazi vizuri ya kuchuja uchafu na sumu mwilini.
Dk Ndugulile ameeleza kuwa mtu mmoja anahitaji kulipa Shilingi za Kitanzania Milioni 37 kama gharama za kusafisha damu nje ya nchi kila mwaka.
Akizungumzia upandikizwaji wa figo, ameeleza kuwa gharama za kupandikiza figo nje ya nchi ni wastani wa Shilingi Milioni 75 hadi 77 kwa mtu mmoja ambayo inajumuisha matibabu hayo ya upandikizaji, nauli pamoja na malazi.
Wafanyakazi wa Dangote wamegoma, RC Mtwara katoa maagizo na maamuzi