Chombo kinachosimamia na kutetea haki za waandishi wa habari nchini Cameroon, kimewashukia na kuwashtaki walinzi wa nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Usafirishaji Alain Edgard Mebe Ngo’o kwa kumdhalilisha mwandishi wa habari.
Inaelezwa kuwa mwandishi huyo alikwenda kutafuta habari nyumbani kwa waziri huyo ambaye alikuwa amefukuzwa kazi siku chache zilizopita baada ya Rais wa nchi hiyo Paul Biya kufanya mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri.
Inadaiwa kuwa walinzi hao wali mlazimisha mwandishi huyo wa gazeti la Le Jour nchini humo kuingia kwenye kibanda cha mbwa baada ya kukerwa na mwandishi huyo aliyekuwa akiuliza maswali kuhusiana na waziri huyo.
Jamaa aliekatwa mapanga kisa kumshika Mbuzi wa tambiko