Leo March 12, 2018 taarifa kutokea nchini Burundi katika Chama tawala cha CNDD/FDD ni kuwa kimemtangaza Rais wa sasa wa taifa hilo Pierre Nkurunzinza kama kiongozi mkuu wa kudumu au kiongozi wa milele ndani ya chama hicho.
Uamuzi wa kumtangaza Nkurunzinza umefikiwa baada ya vikao vya siku tatu vilivyofanyika katika eneo la Buye mahali anapozaliwa Rais Kaskazini mwa Burundi
Uamuzi huo pia unachukuliwa wakati Burundi inajiandaa kufanya marekebisho ya katiba ili kumruhusu Rais Nkurunzinza kuendelelea kuongoza taifa hilo hadi mwaka 2034.
Taarifa ya chama cha CNDD/FDD imesema vikao vimekubaliana kuimarisha chama tawala na taasisi zake.
“HATA WAKIANDAMANA NDANI YA NYUMBA, MTU AKAUMIA, ALIYEITISHA ATAWAJIBIKA” WAZIRI MWIGULU