Baada ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi ‘NACTE’ kusitisha shughuli za kitaaluma kwenye chuo cha uuguzi na Ukunga cha St Glory kilichopo kimara DSM, Uongozi wa chuo hicho wamejitokeza mbele ya wanahabari na kukanusha baadhi ya mapungufu yaliyoainishwa na NACTE na kudai kuwa yamepikwa na wafanyakazi wa chuo hicho wasio waaminifu.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa chuo hicho Felister Massawe “habari ambayo imekuwa ikivuma kwenye vyombo vya habari si ya kweli asilimia mia, kwa sababu wanafunzi wa chuo hiki wamekuwa na walimu tofauti toafuti na sababu ya tofauti ya utumishi iliyotokea humu ndani iliyumbisha chuo”