Kocha wa timu ya taifa ya Brazil Luiz Felipe Scolari amesema kwamba ikiwa timu yake itashindwa kubeba ubingwa wa kombe la dunia basi atakimbilia nchini Kuwait kujificha.
Brazil wamekuwa na maandalizi mazuri tangu walipoweza kutwaa ubingwa wa kombe la mabara mwaka jana, na ni moja ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kubeba ubingwa huo wa dunia baadae mwaka huu.
Scolari, ambaye aliiongoza Brazil kutwaa kombe la dunia miaka 12 iliyopita, ana matumaini anaweza kurudia alichokifanya nchini Korea na JAPAN mwaka 2002, na anaamini ana kikosi kizuri cha kuweza kushindana na timu yoyote.
“Ikiwa sitoweza kubeba kombe la dunia, nitakuwa tayari kuondoka nchi hii niende kupata hifadhi ya kisiasa Kuwait,” kocha huyo wa zamani wa Ureno na Chelsea.
“Tunawaheshimu wapinzani wetu, lakini tupo tayari kupambana na yoyote.”
Brazil wamepangwa kundi moja na Mexico, Croatia na Cameroon katika kundi A katika hatua ya kwanza ya michuano hiyo.