Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa ya Furaha ambayo hutolewa kila mwaka imezinduliwa rasmi kwa mwaka 2018 ambapo kwa mwaka huu imelinganisha nchi 156 kwa kuangalia vigezo mbalimbali.
Vigezo hivyo vilivyotumiwa ni pamoja na matarajio ya maisha (life expectancy), uhuru wa jamii pamoja na kutokuwepo kwa vitendo vya rushwa katika nchi husika zilizolinganishwa.
Katika ripoti hii nchi ya Burundi ndio imetajwa kuwa nchi ambayo watu wake hawana furaha zaidi duniani huku Finland ikitajwa kuwa nchi ya watu wenye furaha zaidi.
Inaelezwa kuwa Burundi imeonekana kuwa na watu wenye huzuni kutokana na machafuko ya kisiasa kutokana na Rais Pierre Nkurunzinza kuchaguliwa kuongoza nchi hiyo kwa msimu wa tatu mwaka 2015.
BREAKING: “Tuzaliane, tufanye kazi la sivyo tutalia tu vyuma vinatubana” JPM