Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo March 14, 2018 ameweka jiwe la msingi la kipande cha pili cha mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge) kinachoanzia Morogoro hadi Makutupora Mkoani Dodoma.
Akizungumza JPM amewataka Watanzania kulipa kodi ili nchi iweze kusonga mbele na kuwaagiza TRA wahakikishe wanakusanya kodi halali na kuacha kuwabambikia wananchi kodi ambayo hawastahili kitu kinachosababisha wengine kukwepa kulipa kodi.