Nchi zote duniani zina utaratibu unaotofautiana na nchi nyingine katika masuala ya elimu na jinsi ya kuwajibisha watoto wanaokataa shule au hata wazazi ambao wanawakosesha watoto wao masomo kwa sababu yoyote ile.
Hatahivyo siku za hivi karibuni, kumetokea jambo ambalo limeshangaza watu duniani kote baada ya wazazi nchini England na Wales kulipishwa faini ya Paundi Milioni 24 sawa na Shilingi za Kitanzania Bilioni 74.4 kwasababu ya kushindwa kuwaandikisha watoto wao shule katika miaka mitatu iliyopita.
Hili limezungumzwa kwa lengo la kufanya wazazi wawe makini na suala la elimu ya watoto wao na kuhakikisha wanawaandikisha shule na wakianza waendelee bila kukomea njiani.
Baada ya Madiwani watatu wa CUF na CDM kuhamia CCM, Mwenyekiti azungumza