Jimbo la Oklahoma nchini Marekani limepitisha rasmi suala la kutekeleza adhabu ya kifo kwa wafungwa nchini humo kwa kutumia gesi ya Nitrogen badala la kunyongwa kama ambavyo ilikuwa awali.
Tangazo hilo lilitolewa na Mwanasheria Mkuu wa jimbo hilo Mike Hunter katika mkutano wa Waandishi wa Habari ambapo alieleza kuwa njia hiyo ya gesi ya nitrogen ni bora zaidi kwani ni rahisi kupatikana na hupelekea kifo kisicho cha maumivu.
Inaelezwa kuwa adhabu hiyo ya kifo ilisimama kwa kipindi cha miaka mitatu kutokana na njia iliyokuwa ikitumika ya sindano ya sumu kushindwa kuendelea kutokana na kutopatikana sindano hizo, na hii ni kwasababu watengenezaji walikataa kuziuza kwa matumizi ya kuua wafungwa.
Ndoto anayotamani kuifanya DC wa Muheza, Ameanza na Kampeni hii