Suala la usawa wa kijinsia linaendelea kuzungumziwa duniani kote kwenye sekta mbalimbali za maisha na maendeleo likiendana na suala la kuwawezesha wanawake kushika nafasi mbalimbali ambazo miaka ya nyuma zilikuwa zikishikwa na wanaume.
Kwa mara ya kwanza nchini Australia kwenye jimbo la Tasmania wanawake wengi zaidi ya wanaume wamechaguliwa kuwa wabunge kwenye Bunge la jimbo hilo jambo ambalo limezungumzwa kuwa la kipekee kuwahi kutokea.
Kiongozi wa Chama cha Upinzani Michelle O’Byrne ameliambia Shirika la Utangazaji BBC kuwa suala hilo limefanya mabinti wa nchini humo waone kuwa ndoto zao za kuwa wanasiasa na viongozi wa baadaye zinaweza kutimia.
Katika uchaguzi wa wabunge hao, wanawake 13 na wanaume 12 wamechaguliwa kuwawakilisha wananchi wao bungeni.
Mwalimu wa Mtoto Jasiri aliemshtaki Baba yake Polisi kwa kuuza shamba, kaongea