Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Phantom Secure Vincent Ramos akiwa na wenzake wanne wamehukumiwa kwa mashtaka ya kuuza teknolojia ya simu kwa kampuni na mitandao ya kihalifu ili wafanye mipango ya kusafirisha dawa za kulevya duniani kote bila kukamatwa.
Akitoa taarifa rasmi Mkurugenzi wa FBI Christopher Wray ameeleza kuwa washtakiwa hao walitengeneza huduma ambayo iliwawezesha wahalifu wa ulimwenguni wa dawa za kulevya, kufanya shughuli hizo bila kutambuliwa na vyombo vya usalama.
Inaelezwa kuwa mara ya kwanza Serikali ya Marekani kukamata viongozi ambao wanasaidia wahalifu wa dawa hizo za kulevya kutoshikwa na mkono wa sheria na usalama.
Mwalimu wa Mtoto Jasiri aliemshtaki Baba yake Polisi kwa kuuza shamba, kaongea