Leo March 16, 2018 stori ninayokusogezea ni kuhusu kubainika kuwa vipimo vya maji yanayouzwa katika chupa za plastiki vimebaini kwamba maji hayo yana vipande vidogo vya plastiki ndani yake.
Uchunguzi huo mkubwa kuwahi kufanyika duniani umebaini kuhusu maji hayo kwenye chupa 250 zilizonunuliwa kutoka mataifa 250 na kuchunguzwa.
Utafiti ulioongozwa na shirika la waandishi wa habari Orb Media, ulibaini vipande 10 vya plastiki katika lita moja ya maji, ikiwa ni ukubwa wa upana wa unywele wa binadamu.
Kampuni ambazo maji yao yalichunguzwa ziliambia Shirika la Utangazi BBC kwamba chupa zao za maji zilitengenezwa kwa ubora wa hali ya juu na vipimo hivyo vilifanywa katika chuo cha kitaifa cha New York huko Fredonia.
Sherri Mason ambaye ni Profesa wa kemia katika chuo kikuu alifanya uchanganuzi huo na kuiambia BBC ”tulipata plastiki katika chupa baada ya chupa, hatunyoshei kidole cha lawama chapa fulani, ni kuonyesha tu kwamba hili hufanyika kila mahali , kwamba plastiki imekuwa na ushawishi mkubwa katika jamii na imeingia katika maji ,ambayo hutumika sana katika jamii”
”Kufikia sasa hakuna ushahidi kwamba utumizi mdogo wa plastiki unaweza kukudhuru, lakini kuelewa athari zake ni muhimu sana katika sayansi” –Mason
‘NABII ANAEGAWA HELA SHILLAH’ AZUNGUMZA KANISA KUFUTIWA USAJILI, KUITWA DODOMA
Mwalimu wa Mtoto Jasiri aliemshtaki Baba yake Polisi kwa kuuza shamba, kaongea