Mkurugenzi Mtendaji mkuu wa mamlaka ya maji Jijini Dar es salaam DAWASCO Cyprian Luhemeja amefafanua ni kwanini bili za maji safi zinaonekana kuwa kubwa kwa baadhi ya wananchi.
Akizungumza katika wiki ya maji amesema kinachofanya bili kuwa kubwa ni matumizi ya maji ya sehemu husika ndio yanasababisha bili kuongezeka na sio kwamba wao wanatoza kiwango kikubwa.