Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Mwigulu Nchemba March 16, 2018 amewataka wanafunzi kuachana na harakati za kutengeneza taswira mbaya juu ya serikali badala yake kuwa na mitazamo chanya.
Ameyasema hayo katika kongamano la UNILIFE lililofanyika Chuo cha Biashara (CBE), ambalo liliandaliwa na Mbunge wa Viti Maalum, Ester Mmasi.
Amesema wanafunzi hawatakiwi kufanya harakati ili wawe adui wa serikali kwani serikali yenyewe haina muda wa kushughulikia mashinikizo ya wanafunzi.
“Nilishawahi kufanya harakati nikiwa chuoni na nilipewa jina la Chifu, majina yangu yamekuja kujulikana nikiwa serikalini lakini nilikuwa napinga baadhi ya ajenda za Taifa ambazo niliona hazina manufaa,” – Dk Mwigulu Mchemba.
Baba alieshtakiwa Polisi na Mwanae azungumzia kifo cha Mama Anthony, watoto 20