Siku ya jana March 16, 2018 serikali ya nchini Burundi imewaachia huru wafungwa takriban 720 kwa msamaha wa Rais waliokuwa wamefungwa katika magereza mbalimbali.
Inaelezwa kuwa wengi wao ni wanawake na wanaompinga Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunzinza kwa kile kinachoitwa kutishia ulinzi na usalama wa nchi kutokana a kufanya maandamano kuupinga utawala wake mwaka 2015.
Waziri wa Haki nchini humo Laurentine Kanyana ameeleza kuwa Rais Nkurunzinza ametoa msamaha huo ili warudi nyumbani kwao ikiwa kama ishara ya upatanisho nchini humo.
Baba alieshtakiwa Polisi na Mwanae azungumzia kifo cha Mama Anthony, watoto 20