Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) siku za hivi karibuni imetoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari ikieleza kuwa inatarajia kujenga Makao Makuu mapya ya Jumuiya hiyo.
Inaelezwa kuwa makao hayo makuu yatajengwa na China na mradi mzima utagharimu Dola za Marekani Milioni 31.6 ambayo ni sawa na Shilingi za Kitanzania Bilioni 75.8 na hii itaanza karibuni na tayari jumuiya hiyo na China wamekwisha tia sahihi makubaliano ya maelewano (Memorundum of Undestanding).
Mradi huo unatarajiwa kuhusisha majengo ya ofisi na kumbi za mikutano, ikiwa ni pamoja na miundombinu ya barabara, umeme, maegesho ya magari, vituo vya ulinzi katika eneo maalumu litakalotengwa.
Mwigulu ametamani kumuona Nondo chuoni, aongelea yeye kujiuzulu