Leo March 19, 2018 Vigogo watano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) wanaokabiliwa na shtaka la matumizi mabaya ya madaraka, wamewasilisha hati zao za kusafiria katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Hati hizo zimewasilishwa mbele ya hakimu mkazi mkuu, Wilbard Mashauri huku upande wa mashtaka ukiwakilishwa na wakili wa Serikali, Emmanuel Jacob.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi April 18, 2018 kwa ajili ya kutajwa.
Washtakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ni aliyekuwa mkurugenzi mtendaji, James Mataragio, kaimu meneja wa uvumbuzi, George Seni, mkuu wa kitengo cha ununuzi na utawala, Wellington Hudson, mkurugenzi wa mkondo wa juu, Kelvin Komba na Edwin Riwa ambaye ni kaimu mkurugenzi wa mipango.