Kutoka nchini Marekani taarifa ya kusikitisha ni kuhusiana na mtoto kike wa miaka 13 aishiye Missisipi na familia yake kupigwa risasi na mdogo wake wa miaka 9 hadi kupoteza maisha.
Inelezwa kuwa watoto hao walikuwa wanacheza game ya video ambapo mdogo mtu aliamua kuchukua bunduki baada ya kuona dada yake hataki kuachia controller ya game hiyo.
Mtoto huyo alimpiga dada yake risasi kutokea nyuma na inadaiwa kuwa risasi hiyo iliingia moja kwa moja kwenye ubongo. Hadi sasa haijajulikana jinsi gani mtoto huyo aliipata bunduki hiyo na kama atachukuliwa hatua au la.
BREAKING: Alichozungumza Zitto Kabwe mbele ya waandishi wa habari