Leo March 20, 2018 nakusogezea stori kutoka kwa Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ambapo ametangaza uwezekano wa kuamua kukifunga kisiwa maarufu nchini humo cha Bocaray siku za usoni.
Ameeleza sababu za kutaka kufunga kisiwa hicho kuwa kinapelekea uharibifu wa mazingira na hivyo lengo ni kuepuka athari za uharibifu huo wa mazingira ambao kwa sasa unaendelea katika kisiwa hicho.
Kisiwa hicho cha Boracay kinatajwa kutembelewa na watalii zaidi ya milioni moja na kuingiza mapato ya Dola za Marekani 772.5 ambayo ni sawa na Shilingi za Kitanzania Trilioni 1.8 kila mwaka.
Utafiti wa mwaka 2015 uliofanywa na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japani (JICA) lilionyesha kuwa mwamba wa matumbawe wa kisiwa hicho umeharibiwa sana na shughuli zinazohusiana na utalii.
Utafiti pia umebaini kuwa ubora wa maji katika kisiwa hicho umeharibika sana kutokana takataka zinazotupwa kwenye maji hayo.
Maneno ya Prof Tibaijuka baada ya Rugemalira kuendelea kusota Rumande